Utekaji nyara bado waendelea, vijana wawili zaidi walitekwa nyara jana usiku mtaani South B

  • | Citizen TV
    2,459 views

    Takribani saa 48 baada ya Rais William Ruto kuahidi wakenya kwamba serikali itakomesha utekezaji nyara, uhalifu huo ungali unaendelea. Vijana wawili, Joseph Ombita na Majid Glorie walitekwa nyara katika mtaa wa South B hapa jijini Nairobi jana usiku. Wakenya sasa wakionyesha hisia za kutojua wamgeukie nani atakayewahakikishia usalama wao. Kwa mujibu wa walioshuhudia kisa hicho, wawili hao walikamatwa na watu waliokuwa wamevalia masurupwenye na kuwaingiza ndani ya gari aina ya probox, kisha wakaondoka nao.