- 610 viewsDuration: 1:56Viongozi wa Kenya Kenya Kwanza wanaendelea kutetea Sheria kuhusu udhibiti wa mitandao iliyoidhinishwa na rais William Ruto wakisema kuwa wale wanaopinga sheria hiyo wanawapotosha wakenya. Sheria hiyo imekumbwa na upinzani kwa madai kwamba inalenga kuwanyamazisha wakosoaji wa serikali, japo viongozi wa Kenya kwanza wakiongozwa na Spika wa bunge Moses Wetangula na kiongozi wa wengi bunge la kitaifa Kimani Ichunghwah wakisisitiza kwamba sheria hiyo ni ya kuhakikisha nidhamu inadumishwa katika mitandao ya kijamii. Walizungumza huko Isanjiro eneo Bunge la Malava.