Viongozi wakashifu ukuruba wa serikali na kampuni ya Adani

  • | Citizen TV
    1,595 views

    Kinara wa chama cha Narc-Kenya Martha Karua, kiongozi wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot, aliyekuwa gavana wa Makueni Kivutha Kibwana na mwanasiasa Muhkisa Kituyi wamekashifu vikali ukuruba wa serikali na kampuni ya Adani uliozua utata nchini. Viongozi hao wamesema hiyo ni njama ya kuwafaidisha wachache serikalini na wala sio kwa manufaa ya wakenya. Pia wameitaka tume ya huduma ya polisi kuwajibika kuhusu kaimu inspekta jenerali wa polisi ambaye amekiuka amri za mahakama.