Vita: Wachambuzi wa kisiasa na ulinzi waeleza nini lengo la Putin

  • | VOA Swahili
    426 views
    Wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wakijiandaa kwa mazungumzo ya dharura kuhusu misaada ya kijeshi baada ya utawala wa Trump kusitisha msaada wake kwa Ukraine, wataalam kadhaa wa Russia wanasema kuwa Moscow inajitahidi kuvuruga mshikamano wa Magharibi. Kufuatia majibizano ya wiki iliyopita huko White House kati ya viongozi wa Marekani na wale wa Ukraine, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, Jumatatu aliilaumu Ulaya kwa kuendeleza vita hivyo, akiongeza kuwa marekebisho kwenye sera za mambo ya nje za Marekani kwa sehemu kubwa zinaendana na mtazamo wa Moscow. Maoni hayo yamekuja kabla ya kuanza kwa mkutano wa fedha wa Umoja wa Ulaya Alhamisi ukilenga kuimarisha usalama wa bara hilo pamoja na msaada kwa Ukraine ambayo kwa miongo kadhaa imekuwa ikitegemea msaada wa ulinzi kutoka Marekani. Kwenye mahojiano ya hivi karibuni na gazeti la kijeshi la Krasnaya Zvezda, Waziri wa Mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov alimtaja rais Trump kama “ mtu anayeangalia masuala kwa kina” na kwamba kauli mbiu yake ni “tumia akili.” Alisema kwamba majanga yote ya dunia kwa zaidi ya miaka 500 iliyopita yalianzia au kufanyika Ulaya kutokana na sera zao wakati Marekani ikiwa haijahusika. #trump #zelenskyy #ukraine #russia #voa #makamurais #jdvance #msaada