Waandamajai warushiwa maji ya pilipili Uturuki

  • | BBC Swahili
    312 views
    Serikali ya Uturuki inasema watu 1,133 wamekamatwa katika siku tano za maandamano kote nchini - machafuko mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja. Maandamano yalianza wakati Meya wa Istanbul Ekrem Imamoglu - mpinzani wa Rais Erdogan - alipowekwa kizuizini siku ya Jumatano kwa tuhuma za rushwa. Imamoglu anasema mashtaka hayo yamechochewa kisiasa, jambo ambalo Erdogan anakanusha. Uchaguzi wa rais wa Uturuki utafanyika 2028 - Imamoglu alithibitishwa Jumatatu kuwa atagombea kupitia chama chake. #bbcswahili #Uturuki #maandamano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw