Waandamanaji wa rika la Gen Z kaunti ya Mombasa waendeleza shinikizo la kupinga uteuzi wa mawaziri

  • | K24 Video
    285 views

    Waandamanaji wa rika la Gen Z kaunti ya Mombasa wameendeleza shinikizo la kupinga uteuzi wa mawaziri waliohudumu katika baraza lililovunjwa na sasa wanawashinikiza wabunge wasiowaidhinishe wakati wa usaili. Maandamano ya waandamanaji hao yaliyoanza maeneo ya pembe za ndovu yalitibuliwa na polisi muda mfupi baada ya kuanza. Maafisa wa polisi walikuwa wameimarisha usalama katika maeneo mengi.