Waandishi wajituma kuufahamisha umma kuhusu habari potofu za Mpox, COVID-19

  • | VOA Swahili
    40 views
    "Mjini Kinshasa, ninapoishi, nimegundua kwamba kuna hali ya kutojali kuhusu raia kupambana na virusi vya Corona kwa sababu watu wengi hawaamini kwamba kuna ugonjwa huo idadi kubwa ya watu wasioamini kwamba kuna ugonjwa ni wale wanaoishi nje ya mji," J. Kazimoto. Naye Daniel Makeke ni mhariri. Anasema juhudi hizo ni muhimu katika kupambana na habari potofu. Vituo vya radio vinategemea podcasts ili kueneza taarifa kuhusu magonjwa na majanga, namna ya kupata tiba, ukweli kuhusu tiba na chanzo cha monkeypox, miongoni mwa mengine. Kwa namna hiyo, tunaweza hata kuwafikia watu wasiokuwa na uwezo wa mtandao wa kidijitali ambao wanafaidika na kazi yetu ya kutafuta ukweli. Makeke anasema juhudi za Eleza ukweli zinasaidia kuzuia kusambaa kwa habari za uongo kuhusu magonjwa kusambaa, zinazoweza kuwa hatari kwa afya. Mwandishi wa habari Zanem Nety Zaidi ameandaa ripoti hii kutoka Goma, DRC. #habaripotofu #drc #goma #waandishi #voa #voaswahili #covid19 #mpox #virusi