Waasi wa Syria wakiingia katika mji mkuu, Damascus

  • | VOA Swahili
    575 views
    Kanda ya video inawaonyesha waasi wa Syria wakiingia katika mji mkuu, Damascus. Video hiyo inaonyesha vikundi vya watu wenye silaha wakiwa katika magari madogo na malori yanayopita mjini na wengine wakitembea kwa miguu mitaani, huku milio ya risasi ikifyatuliwa hewani kiholela. Waasi hao walitangaza Jumapili kuwa walikuwa ‘wameikomboa Damascus’ na kumpindua Rais Bashar al-Assad. Wakati huo huo, jeshi la Syria lilisema kuwa linaendelea na operesheni dhidi ya ‘vikundi vya magaidi’ katika miji ya Hama na Homs, na pia nje ya mji wa Deraa. (AP) #syria #damascus #alassad #voa