Wabunge 44 wapiga kura kupinga hoja dhidi ya Gachagua

  • | Citizen TV
    1,236 views

    Kabla ya kupiga kura ya kuunga mkono hoja ya kumuondoa ofisini Rigathi Gachagua, wabunge walijadili kwa mihemko mienendo, tabia na matamshi ya Gachagua ambayo wanasema ni ya kudhalilisha. Wabunge hao walimshambulia Gachagua kwa kujinufaisha kupitia ufisadi, mali ambayo si yake, matamshi ya kudhalilisha wanawake na pia kukiuka katiba kwa kumpuuza au kumdhalilisha rais William Ruto.