Wadau wa utunzaji wa msitu wa Kirisia, Samburu washinikiza vijana kuajiriwa

  • | Citizen TV
    226 views

    Shirika la kijamii la kulinda na kuhifadhi misitu la Kirisia katika kaunti ya Samburu, limeirai serikali kuwaajiri walinzi na maskauti wa misitu wa kujitolea, hasa wale wanaoendeleza juhudi za uhifadhi wa misitu. Wadau hao wanaitaka serikali kuwapa kipaumbele vijana hao kwenye nafasi za ajira za huduma za wanyamapori na huduma za misitu KFS.