Wafanyabiashara humu nchini wamehimizwa kutumia fursa ya maonesho ya bidhaa za China , Canton Fair

  • | KBC Video
    9 views

    Wafanyabiashara humu nchini wamehimizwa kutumia fursa ya maonesho ya bidhaa za China al-maarufu Canton Fair kuagiza bidhaa bora na kupata masoko mapya ili kuimarisha ubia wa kibiashara na Uchina . Akiongea jijini Nairobi wakati wa kikao kilichowaleta pamoja wadau wa sekta ya biashara, mwenyekiti wa masuala ya biashara na udiplomasia katika chama cha kitaifa cha wenye biashara na viwanda humu nchini, Ronald Meru amesema maoneesho hayo yatawaunganisha moja moja wanabiashara wa Kenya na wasambazaji wa bidhaa katika masoko ya kimataifa hayo yakiwa mojawapo ya maonesho jadi yanyoandaliwa mara mbili kwa mwaka.Maonesho hayo yatafanyika katika jimbo la Guanzou kati ya tarehe 15 mwezi Aprili na tarehe tano Mwezi Mei mwaka huu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive