Wafugaji wa samaki Busia wakadiria hasara baada ya kushindwa kuendeleza kilimo hicho

  • | Citizen TV
    293 views

    Wafugaji wa samaki katika vidimbwi vya Bukani vilivyoko katika eneo bunge la Funyula kaunti ya Busia wanakadiria hasara baada ya kushindwa kuendeleza kilimo hicho kwa zaidi ya miaka mitatu sasa kwa kukosa fedha.Mradi wa zaidi ya shilingi milioni 60 wa Bukani wenye vidimbwi 100 ulianzishwa katika mashamba ya wakulima hao kwa ushirikiano wa serikali ya kaunti ya Busia na ufadhili wa Benki ya Dunia.