Wahalifu wawili zaidi wakamatawa kaunti ya Mombasa

  • | Citizen TV
    1,695 views

    Washukiwa wawili zaidi wa uhalifu wametiwa mbaroni usiku wa kuamkia leo na kuongeza idadi ya waliokamatwa katika msako huko Mombasa kufikia watu 165. Kamanda wa polisi eneo la mvita Maxell Agoro amesema msako huo utaendelea baada ya kamera za cctv kubaini kuwa genge la vijana limekuwa likiwapora wakazi kisiwani Mombasa.