Waititu ahukumiwa miaka 12 jela akishindwa kulipa faini ya shilingi milioni 53.5

  • | K24 Video
    182 views

    Aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu atalazimika kutumikia kifungo cha miaka 12 gerezani kuanzia usiku endapo atashindwa kulipa faini ya shilingi milioni 53.5. hakimu mkuu wa mahakama ya kupambana na ufisadi ya milimani, Thomas Nzioka ametoa uamuzi huo baada ya waititu na mkewe kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa fedha na utumizi mbaya wa ofisi. Mkewe alitakiwa kutumikia kifungu cha mwaka mmoja au faini ya shiling nusu milioni. Hatahivyo mkewe ameachilia baada ya kulipa faini hiyo.