- 467 viewsDuration: 4:36Kuboreshwa kwa huduma na kuwepo kwa mashine za kisasa katika hospitali ya level 4 ya Amukura iliyoko katika eneo bunge la Teso ya kati kaunti ya Busia kumesaidia kubaini kwa haraka magonjwa sugu yanayowatatiza wakazi wa eneo hilo. Visa vya ugonjwa wa selimundu na kifafa vinazidi kunakiliwa kwa kasi katika hospitali hiyo ya rufaa, idadi ya waliopimwa na kupatikana na chembe chembe za selimundu ikifikia 78 kwa muda wa miezi mitatu.