Wakaazi wanalalamikia kutapakaa kwa taka Diani

  • | Citizen TV
    510 views

    Wakaazi na wafanyibiashara wa mji wa kitalii wa Diani wamelalamikia serikali ya kaunti ya Kwale na manispaa ya Diani kwa kutozoa taka zilizorundika katikati wa mji huo.Mapipa ya taka yaliowekwa sehemu tofauti mjini humo yamejaa na taka kutapakaa ovyo kwa takriban miezi miwili sasa. wakaazi wanahofia mlipuko wa magonjwa haswa katika msimu huu wa mvua. Lawrence Ng'ang'a anaarifu zaidi kutoka Kwale.