Wakulima wa miwa wa maeneo ya magharibi na Nyanza wakasirishwa na uamuzi wa jaji Chacha Mwita

  • | K24 Video
    47 views

    Wakulima wa miwa wa maeneo ya magharibi na nyanza wamekasirishwa na uamuzi wa jaji Chacha Mwita wa kutupilia mbali kesi ya kupinga uamuzi wa serikali wa kukodisha viwanda vinne vya umma kwa kampuni za kibinafsi. Wadau wamesema uamuzi huo utawapokonya wakulima haki ya kupigania maslahi yao na kupoteza uwezo wa kudhibiti bei ya sukari. Hatahivyo serikali inasema kuwa ubinafsishaji wa viwanda vya sukari utaimarisha utendaji, utapunguza madeni na utahuisha sekta ya sukari inayoyumba. Wakulima hawana uhakika wa mtazamo huo