- 264 viewsDuration: 2:03Hatua ya wizara ya elimu ya kufunga na kuhamishia wanafunzi wa shule ya msingi ya Hatata kaunti ya Tana River hadi shule jirani ya Anole imeanza kukera wazazi wa shule hiyo baada ya wanafunzi wengi kusitisha masomo. Kulingana na wazazi hao shule hiyo ilifungwa mwaka jana kutokana na athari ya mafuriko kama njia ya dharura ya kuokoa hali ya elimu ya watoto wao lakini hakuna suluhu ya kudumu ilitolewa na wizara hadi kufikia sasa. Kutokana na umbali wa shule jirani, wanafunzi wameanza kuingilia biashara ya kuuza vyuma vikukuu na chupa za plastiki huku wasichana wapachikwa mimba na wingine kuozwa mapema.