Skip to main content
Skip to main content

Wasichana wageuzwa kuwa kipato Kaskazini ya nchi kufuatia baa la njaa

  • | KBC Video
    439 views
    Duration: 5:19
    Huku meno ya ukame yakizidi kung’ata bila huruma eneo la Kaskazini ya taifa, hali ya utamaufu inazilazimu familia kufanya maamuzi mazito. Katika eneo la North Horr kaunti ya Marsabit, baadhi ya wazazi wanawaoza wasichana wao wadogo, baadhi yao wakiwa ndio wanaanza kubaleghe ilmuradi wazazi hao wakwepe kinywa cha mauti. Mifugo wameangamia, chakula ni adimu kupatikana na kwa wengine mahari pekee ndio yamesalia kuwa biashara ya kujadiliwa. Ni watoto ambao wamejipata katika mtanziko wa utamaduni, umaskini pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi. Leo usiku, katika shajara ya matukio ya ukame, ripota wetu Ben Chumba anatupa taarifa yakinifu kutoka Marsabit kuhusiana na jinsi janga la ukame limesababisha balaa na beluwa kwa wasichana wadogo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive