Wasifu wa Wafula Chebukati

  • | Citizen TV
    0 views

    Kilele cha utendakazi wa wakili wa muda mrefu Wafula Chebukati kiliwadia katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022, alipotangaza William Ruto kuwa rais. Rais Ruto aliwahi kumtaja Chebukati kama shujaa wa uchaguzi huo. Hata hivyo upande wa upinzani wakati huo ukiongozwa na Raila Odinga uliamini kuwa Chebukati alikuwa kizingiti katika nafasi yao ya kuliongoza taifa. Alipoongoza tume ya IEBC, Chebukati alikabiliana na majaribio si haba, akiyumbishwa na mawimbi ya kisiasa yaliyomwachwa mpweke, makamishna wanane wakitofautiana naye alipokuwa mwenyekiti, lakini akaandikisha historia kuwa mwenyekiti wa kwanza wa IEBC kukamilisha muhula wake wa miaka sita.