Idadi ya watu waliopoteza makazi kufuatia ongezeko la maji kwenye Ziwa Naivasha imefikia 4,000 huku kukiwa na wasiwasi kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na mvua inayoendelea kunyesha. Tangu mwanzo wa mwaka huu, viwango vya maji katika Ziwa Naivasha vimekuwa vikiongezeka na hali imekuwa mbaya zaidi katika muda wa miezi mitatu iliyopita. Maji hayo yamefurika kwenye nyumba za makazi, vyoo, shule, makanisa na hata kituo kimoja cha polisi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive