Watu kumi waaga dunia kutokana na ajali ya barabarani eneo la Chemoset kaunti ya Uasin Gishu.

  • | Citizen TV
    1,529 views

    Kulingana na polisi, gari la abiria liligongana ana kwa ana na lori saa moja asubuhi, ambapo watu tisa walifariki papo hapo na mwingine kufariki akipelekwa hospitalini. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, wakazi wa eneo la Soi wameitaka serikali kuimarisha barabara ya Kitale kuelekea Eldoret wakidai kuwa imesbabisha ajali nyingi kutokana na wembamba wake.