Wazee wa jamii ya Agikuyu watakasa barabara ya Nairobi-Nakuru

  • | KBC Video
    240 views

    Wazee wa jamii ya Agikuyu chini ya mwavuli wa kundi la Kiama Ki'ama hii leo walikita kambi kwenye barabara kuu ya kutoka Nairobi kuelekea Nakuru kwa saa kadhaa, kwa hafla ya kutakasa barabara hiyo kufuatia msururu wa ajali. Wakiongozwa na Muthamaki Thiong'o Wa Gitau, wazee hao waliomba neema kutoka kwa Maulana huku wakitoa wito kwa serikali ya kitaifa, kuharakisha ujenzi wa barabara ya safu mbili ili kupunguza ajali. Hafla hiyo inajiri kufuatia vifo vya zaidi ya watu 10 katika muda wa siku nne kwenye barabara hiyo. Timothy Kipnusu na mengi zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive