- 3,815 viewsDuration: 2:50Idara ya upepelezi wa jinai imesema kuwa picha za CCTV zimebainisha sekunde za mwisho kabla ya waziri wa zamani Cyrus Jirongo kuaga dunia kwenye ajali ya ana kwa ana katika barabara kuu ya Nakuru–Nairobi ikisema kuwa ajali hiyo ilitokea sekunde 25 baada ya saa nane usiku. Kwenye taarifa idara ya DCI sasa imethibitisha kwamba ajali hiyo ilihusisha basi la uchukuzi wa umma ambapo dereva wake amehojiwa na kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu huku wapelelezi wa mauaji na wataalamu wa uchunguzi wa maiti wakichanganua mienendo yake yote ikiwemo mahali alikokuwa awali usiku huo kabla ya kuwasilisha taarifa kamili kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive