- 23,084 viewsDuration: 4:24Mwanzilishi wa kanisa la Zion Fire Annoiting Ministries amekana kuwa dhehebu hilo linajihusisha na imani potovu. Elizabeth Kadori anayesakwa ma polisi huko Mombasa ili kuandikisha taarifa anasema jumapili walikuwa na kesha ya kawaida na kutokana na changamoto za kiusalama wafuasi wa kanisa hilo ikiwemo watoto walisalia katika kanisa hilo hadi asubuhi kabla ya maafisa wa polisi kufika na kuwakamata. Mamia ya wafuasi wa kanisa hilo walimiminika nje ya kanisa hilo wakitaka maafisa wa polisi kutoa ushahidi.