Guinea: Darzeni wafariki wakiwemo watoto kufuatia vurugu katika mechi ya kandanda

  • | VOA Swahili
    543 views
    Uamuzi wa kutatanisha wa refa katika mechi ya mpira wa miguu ulizua vurugu na mkanyagano katika mechi moja ya soka kusini mashariki mwa Guinea, na kuuwa watu 56 kulingana na idadi ya awali, serikali ilisema Jumatatu. Uamuzi wa kutatanisha wa refa katika mechi ya mpira wa miguu ulizua vurugu na mkanyagano katika mechi moja ya soka kusini mashariki mwa Guinea, na kuua watu 56 kulingana na idadi ya awali, serikali ilisema Jumatatu. Vifo vilitokea wakati mechi ya fainali ya mashindano ya kumuenzi kiongozi wa kijeshi wa Guinea Mamady Doumbouya katika uwanja wa michezo huko Nzerekore, mojawapo ya miji mikubwa ya taifa hilo. Baadhi ya mashabiki walirusha mawe, jambo ambalo lilizua hofu na mshtuko, taarifa ya serikali ilisema, na kuahidi uchunguzi. Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina afisa mmoja wa mji huo alisema waathirika wengi walikuwa Watoto waliojikuta katika ghasia hizo baada ya polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi. Afisa huyo alielezea matukio ya mkanganyiko na vurugu huku baadhi ya wazazi wakichukua miili kabla ya kuhesabiwa rasmi. - Reuters #guinea #football #voa