Wanafunzi waliotia fora wataka serikali kufadhili elimu ya juu

  • | Citizen TV
    400 views

    Huku furaha ikiendelea kutawala miongoni mwa wanafunzi na shule zilizopata matokeo bora kwenye mtihani wa kitaifa wa KCSE, mjadala mkali unaibuka kuhusu mustakabali wa elimu ya juu nchini. Wadau wa sekta ya elimu wameshikilia msimamo kwamba ni lazima serikali itoe ufadhili wa kutosha kwa wanafunzi wote waliostahili kujiunga na vyuo vikuu, ili ndoto zao zisitoweke kwa sababu ya ukosefu wa fedha.