Mwanamke apigwa na kujeruhiwa na jirani, Kisii

  • | Citizen TV
    689 views

    Mwanamke mmoja, mama ya watoto watatu analilia haki huko Bomachoge Borabu baada ya kupigwa kinyama na jirani yake kwa madai ya kuiba unga wa ngano. Kisa cha kushambuliwa kwa Mama huyo mwenye umri wa miaka 34 kilisambaa kwenye mitandao baada ya kurekodiwa kwenye kanda ya video.Maafisa wa polisi wamethibitisha kuanzisha msako wa mwanaume huyo akitarajiwa kufunguliwa mashtaka.