Baba dhalimu homabay : Adaiwa kumuua bintiye mchanga

  • | KBC Video
    12 views

    Maafisa wa polisi katika kaunti ya Homa Bay wanamzuilia mwanamme wa umri wa miaka-38 anayedaiwa kumuua bintiye wa umri wa miaka saba kwa kumlazimisha kunywa lita moja ya mafuta ya petroli. Mshukiwa huyo alitoweka pindi alipotekeleza unyama huo mnamo Jumatatu nyumbani kwake kijijini Minyere kata ndogo ya Kanyikela Kusini kaunti ndogo ya Ndhiwa. Baadaye alijisalimishakatika kituo cha polisi kwa Homa Bay ambapo alikamatwa. Akithibtisha kisa hicho, kamishna wa kaunti ya Homa Bay Moses Lilan alisema mwili wa msichana huyo uliokuwa umeanza kuoza ulipatikana jumanne asubuhi huku kukiwa na chupa ya mafuta ya petroli kando yake.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive