Rais Ruto amfurusha waziri Justin Muturi kutoka kwa baraza lake la mawaziri

  • | K24 Video
    2,461 views

    Hatimaye Rais William Ruto amemfurusha waziri wa utumishi kwa umma Justin Muturi kutoka kwa baraza lake la mawaziri. kupigwa kalamu kwa muturi kunajiri saa chache baada ya Rais Ruto kumsuta muturi kwa kile alichokitaja kukosoa kujua kazi alipohudumua kama mwanasheria mkuu. Muturi kwa muda sasa amekuwa akiikashifu serikali sio tu kuhusiana na utekaji nyara bali pia utekelezaji wa miradi tofauti.