Mawakili wa Tundu Lissu wapinga kesi kusikilizwa mtandaoni

  • | BBC Swahili
    10,847 views
    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam hii leo imesikiliza upande wa Jamhuri juu ya hoja za mawakili wa Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Tundu Lisu, ambao walipinga hatua ya kesi kusikilizwa kwa njia ya mtandao. Hapo awali, mahakama ilitoa taarifa kuwa kesi ya uhaini inayomkabili Lisu itasikilizwa kwa njia ya mtandao. Ulinzi uliimarishwa nje ya mahakama huku waandishi wa habari na wafuasi wa chadema wakizuiliwa kuingia ndani ya mahakama. #tundulissu #tanzania #bbcswahili #bbcswahilileo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw