Serikali imesema haijafanikiwa kuupata mwili wa marehemu John Ogutu, mwalimu Mkenya aliyepigwa risasi na kuuawa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Tanzania. Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi amesema Ogutu alifariki kwenye kituo cha kibishara cha Goba kilichoko wilaya ya Ubungo jijini Dar Es Salaam. Wakenya wengine wanane waliokuwa wamekamatwa na kuzuiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi nchini Tanzania hatimaye wameachiliwa huru. Serikali imekuwa ikishinikizwa kushughulikia kutoweka kwa wakenya ughaibuni, wakiwemo waliopelekwa kusaidia majeshi ya Urusi nchini Ukraine.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive