Viongozi kaunti ya kajiado waombwa kuendesha kampeni safi bila matusi

  • | Citizen TV
    373 views

    Huku siasa za uchaguzi mkuu wa tarehe 9 Agosti zinachacha katika sehemu tofauti za nchi, wakaazi wa Kajiado wameombwa kudumisha amani na kutumia lugha nzuri inayodumisha amani. Viongozi katika hafla tofauti za kisiasa wamewasihi wanasiasa pamoja na wapiga kura kufanya kampeni yao bila matusi. David Nkedianye ambaye anawania kiti cha ugavana kaunti ya kajiado,ametaka Idara ya NCIC kuchunguza wanasiasa wanatoa uchochezi ya kupiganisha watu.