Israel yashambulia Rafah wakati mazungumzo ya kusitishwa mapigano yakiendelea

  • | VOA Swahili
    393 views
    Israel imefanya mashambulizi ya angani Alhamisi Rafah iliyoko kusini mwa Gaza baada ya kutishia kupeleka majeshi kupambana na wanamgambo wa Hamas katika mji huo ambapo Wapalestina milioni 1.4 wametafuta hifadhi. Mataifa yenye nguvu duniani yanayoendelea kutafuta njia ya kumaliza vita vya Israel na Hamas hadi sasa yamefeli kufikia hilo, lakini mjumbe mmoja wa Marekani alikuwa anatarajiwa kuwasili Israel Alhamisi katika juhudi za hivi karibuni kutafuta kufikia makubaliano ya kusitishwa mapigano. Vita hivyo pia vimezua kuongezeka kwa ghasia katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi, ambapo Wapalestina wenye silaha walifyatua risasi Alhamisi katika magari yaliyokuwa yamesongamana kwenye barabara kuu, na kumuua mtu moja na kujeruhi wengine nane akiwemo mama mjamzito. Washambuliaji hao waliuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la tukio hilo, karibu na maeneo yanayokaliwa na walowezi wa Kiyahudi mashariki ya Jerusalem. Wanasiasa wa mrengo wa kulia zaidi mara moja walitoa wizo kwa raia zaidi kubeba bunduki na pia kuwepo vizuizi zaidi kwa wakazi wa Kipalestina huko Ukingo wa Magharibi. Israel imeonya kuwa, iwapo Hamas haitawaachia huru mateka waliosalia wanao shikiliwa Gaza ifikapo mwanzo wa mfungo wa Ramadhani, itaendelea kupigana wakati wa mwezi mtukufu wa Waislam, mapigano hayo yakiwa pia eneo la Rafah. Israel tayari imekuwa ikishambulia kwa mabomu malengo huko Rafah, ambapo kwa mara nyingine eneo hilo lilipigwa usiku kucha na mapema Alhamisi waandishi wa AFP walisikia milio kadhaa ya mashambulizi ya angani. “Niliamka na kusikia mlipuko mkubwa kama vile tetemeko la ardhi – moto, moshi na milipuko na vumbi lilikuwa kila mahali,” alisema al-Shaer, mwenye umri wa miaka 21, akieleza yeye na wengine walikuwa wakiwaondoa wanafamilia waliojeruhiwa kutoka ndani ya kifusi. Aliishutumu Israel “haijali chochote” kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu kusitishwa mapigano na badala yake “inataka kuwaondoa watu kutoka Rafah na wanajitayarisha kufanya mashambulizi ya ardhini”.\ Shirika la Civil Defence la Gaza limeripoti “watu kadhaa waliokufa shahidi” huko, wakati kwengineko huko Rafah wakazi walikuwa wakizunguka katika kifusi cha Msikiti wa al-Faruq wa mji huo, baada ya mashambulizi kadhaa. Wakati huo huo China na Iran zimehutubia mahakama ya juu ya umoja wa mataifa kuhusu uhalali wa sera za Israel katika maeneo inayo yakalia kimabavu. Alhamisi ilikuwa siku ya nne ya vikao katika mahakama ya Kimataifa ya haki mjini The Hague kusikiliza ombi la baraza kuu la umoja huo, kutafuta ushauri kuhusu mgogoro wa muda mrefu kati ya Israel na Palestina kuhusu maeneo yanayokaliwa kimabavu. Mwanasheria wa China wa masuala ya mambo ya nje Ma Xinmin, amesema kwamba vita vya sasa katika ukanda wa Gaza ni sehemu ya ukandamizaji wa muda mrefu wa Israel dhidi ya Wapalestina. Iran nayo imedai kwamba Israel inafanya uhalifu katika ukanda wa Gaza. Vikao vya mahakama hiyo vinaendelea siku moja baada ya Marekani kutaka mahakama hiyo kutotoa ushauri wake kwamba Israel inastahili kuondoka katika maeneo hayo inavyotaka Palestina. Vita vilivyoanzishwa na shambulizi la Hamas huko Kusini mwa Israel Oktoba 7 ambapo watu 1,200 waliuawa na wengine 253 kutekwa, kulingana na Israel.⁣ Takriban Wapalestina 29,092 wameuawa na wengine 69,028 wamejeruhiwa hadi sasa. - Vyanzo mbalimbali ikiwemo AFP, AP, VOA #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #iran #iraq #yemen #aden #wahouthi #bahariyasham #msikiti #israel