BBC News Swahili

  • | BBC Swahili
    615 views
    Mtaalamu wa Umoja wa mataifa ameonya kwamba jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur huenda likakumbwa na tishio la mauaji ya halaiki. - Alice Nderitu mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na masuala ya kuzuia mauaji ya halaiki ameiambia BBC kwamba kikosi maalum cha kijeshi cha Rapid Support Force kinalenga jamii kulingana kabila na rangi. - Amesema kwamba mashambulizi yanayozidi kushuhudiwa katika mji wa El Fasher uliopo kaskazini mwa Darfur, ambao ulikuwa mji wa mwisho chini ya uongozi wa vikosi vya jeshi la Sudan (SAF), umekuwa ndio eneo la hivi punde unaofungua upya vita kati ya makundi hayo mawili. - Ghasia na vurugu imekuwa hali ya kawaida ya Maisha huko sasa. - Mtangazaji @bbcswahili Laillah Mohammed anawasilisha taarifa ifuatayo ambapo BBC imezungumza na baadhi ya waathiriwa ndani ya Sudan. - - #bbcswahili #sudan #ghasia #darfur #vita #bbcswahili