Wakulima Garissa wanadai bwanyenye mmoja anatishia kuwafurusha

  • | Citizen TV
    392 views

    Wakulima mjini Garissa, wanalilia haki baada ya bwanyenye mmoja kudaiwa kutishia kuwafurusha kutoka kwenye kipande chao cha ardhi. Wakulima hao ambao ni wanachama wa shamba la Maramtu wanadai kuwa bwanyenye huyo ana mazoea ya kuwatumia maafisa wa polisi kuwatishia kuhama kutoka kwenye shamba hilo la hekari 150 ambalo wanasema walirithi kutoka kwa mababu zao.Wanasema wamejenga makaazi yao ya kudumu kwenye kipande hicho na hawatakubali kufurushwa.Sasa wanataka wakuu wa usalama kuingilia kati na kuzuia maafisa wake kutumiwa vibaya huku wakitafuta haki mahakamani.