Baraza la walemavu laanzisha utafiti kubaini kinachosababisha ulemavu kwa watoto Kwale

  • | Citizen TV
    191 views

    Baraza la walemavu nchini na mashirika ya kijamii kaunti ya Kwale wameanzisha mchakato wa kufanya utafiti kuhusu kinachosababisha baadhi ya watoto kuzaliwa na ulemavu wa kupooza ubongo.Utafiti huo unaaminika kuwa utasaidia jamii kuweka mipango ya kuwakinga watoto kabla ya kuzaliwa. Kaunti ya Kwale tayari ina zaidi ya watoto 3,140 wenye ulemavu huo.