Familia inadai mwili ni tofauti na wa jamaa yao

  • | Citizen TV
    1,043 views

    Mtafaruku umeibuka kuhusiana na mwili unaodaiwa kuwa wa Evans Owino aliyepotea Novemba mwaka jana. Familia yake inahofia kuwa mabaki ya mwili waliopokezwa katika makafani ya Nairobi sio ya mpendwa wao. Familia hiyo ambayo inataka uchunguzi wa DNA kufanywa inasema kuwa mwili uliotambuliwa kupitia alama za vidole ni tofauti na ule waliopewa kwenda kuzika.