- 2,915 viewsDuration: 1:21Baraza kuu la uongozi la chama cha Jubilee limemuidhinisha aliyekuwa waziri wa usalama, Fred Matiang’i, kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi wa mwaka 2027. Mkutano huo ulipokea rasmi na kuidhinisha ombi lake la kuwania kiti cha urais kama mgombea wa chama hicho. Kinara wa chama hicho, rais mstaafu Uhuru Kenyatta aliendesha mkutano huo kwa njia ya mtandao ambapo Matiang’i pia aliteuliwa kuwa mmoja wa manaibu vinara wanne wa chama hicho