Kabogo ataka bunge kutengea mfumo wa kidijitali fedha zaidi

  • | KBC Video
    119 views

    Ajenda ya serikali ya kuweka huduma zake kwenye mfumo wa kidijitali inakabiliwa na upungufu wa ufadhili huku waziri wa habari na teknolojia ya mawasiliano William Kabogo, akionya kwamba kupunguzwa kwa fedha kwenye bajeti, kutachelewesha miradi muhimu. Kabogo aliyekuwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano, alitoa wito kwa wabunge kutenga shilingi bilioni 5.4 zaidi ili kuendeleza sekta ya utangazaji na mawasiliano ya simu, huku wasiwasi ukiongezeka kuhusiana na miradi iliyokwama na mashirika ya serikali yanayokabiliwa na changamoto za kifedha.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News