Kijana aliyepigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya Gen Z aaga dunia Kirinyaga

  • | Citizen TV
    2,096 views

    Kijana aliyekuwa amelazwa hospitalini kwa zaidi ya miezi minane baada ya kupigwa risasi wakati wa maandamano ya Gen Z nchini ameaga dunia. John Mwangi aliyepigwa risasi eneo la Kirinyaga amefariki hospitali ya Kenya alikokuwa akipokea matibabu kwa muda huu wote. Na kama Laura Otieno anavyoarifu, familia ya Mwangi iliyolalamikia kutelekezwa na walioahidi kuwasaidia sasa wanadai haki ya kifo cha jamaa yao