Kituo kipya cha matibabu chajengwa Machakos

  • | KBC Video
    4 views

    Serikali ya kaunti ya Machakos imefungua kituo cha afya kilichojikita katika hospitali ya Machakos Level -5 katika juhudi za kuimarisha huduma za afya katika kaunti hiyo.Gavana wa kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti amesema kituo hicho kinanuiwa kukomesha msongamanao wa wagonjwa na kuwapa nafasi wataalamu wa afya kushughulikia hali za afya zinazohitaji matibabu maalum. Ndeti alisema kucheleweshwa kwa utekelezaji wa halmashauri ya Afya ya Jamii, SHA, kumesababisha changamoto katika mfumo wa kugharamia matibabu. Alisisitiza haja ya kuharakishwa kwa mchakato wa kuwianisha mfumo wa afya wa serikali za kaunti na ule wa halmashauri ya SHA ili kuboresha utoaji huduma.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive