MATANGAZO YA SERIKALI
Wabunge wanataka kujua ni kwa nini mashirika ya serikali yameshindwa kulipa ada zao kwa shirika la serikali la kutoa matangazo, hali ambayo imeathiri shirika hilo kifedha. Katibu katika wizara ya utangazaji Steven Isaboke alipofika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu uhasibu wa umma, alisema haya yanatokana na kiwango kidogo cha mapato kinachotokana na mashirika hayo na kuchelewa kwa mashirika mengine kulipia matangazo yao. Isaboke pia alifichua kwamba wizara hiyo iko katika harakati za kuboresha vifaa katika shirika la utangazaji la Kenya - KBC ili kukuza uwezo wake wa kukusanya mapato.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive