Machifu 5 watekwa nyara na watu wanaoaminika kuwa wanamgambo wa Al Shabaab Mandera

  • | Citizen TV
    1,123 views

    Ripoti kutoka mpakani zinaarifu kuwa machifu watano wametekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab katika kaunti ya Mandera. Maafisa wa usalama wanaripoti kuwa machifu hao walikuwa wakisafiri kutoka eneo la Wargadud kuelekea Elwak kwa kazi. Operesheni ya kiusalama imeanzishwa eneo hili kuwasaka washukiwa wanaoaminika kutorokea taifa jirani la Somalia. Uvamizi huu wa leo umejiri huku Rais William Ruto akipangiwa kufanya ziara katika maeneo ya kaskazini mashariki ikiwemo kaunti hii ya Mandera.