- 957 viewsDuration: 2:26Inspekta jenerali wa polisi ndiye mwenye mamlaka ya kuwaajiri, kuwafuta na kuwahamisha maafisa wa polisi. Haya ni kwa mujibu wa mahakama ya leba ambayo imetoa uamuzi huo kufuatia mgogoro kati ya Tume ya Kitaifa ya huduma za polisi NPSC - na idara ya polisi. Mahakama imesema kuwa NPSC haina mamlaka ya kuajiri maafisa wa polisi na kubatilisha tangazo la zoezi la usajili wa makurutu. NPSC pia imepigwa marufuku kupandisha cheo maafisa wa polisi