Makamu Rais Vance ahojiwa iwapo kukata msaada kwa Ukraine kunaipa nguvu Russia?
Baada ya mkutano wa Ijumaa iliyopita kati ya Rais Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ambao uligeuka malumbano makali, na Rais Tump kusitisha kwa muda misaada ya kijeshi kwenda Ukraine, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance ameweka wazi msimamo wa Marekani kuhusu kumaliza vita vya miaka mitatu kati ya Russia na Ukraine.
Katika mahojiano na VOA, JD Vance aliulizwa ikiwa kusimamisha misaada kwa Ukraine kunaipa fursa nzuri Russia.
Vance amesema lengo la Rais Donald Trump kuhusu sera ya Marekani kwa Ukraine ni kuwaleta raia wa nchi hiyo kwenye meza ya mazungumzo.
Amesema wanataka Waukraine wawe na nchi inayojitawala na huru, akiongeza kuwa majeshi ya Ukraine yamepigana kwa ujasiri mkubwa, lakini wamefikia mahali ambako si Ulaya wala Marekani ambao wanaweza kuendeleza vita hivyo bila ya ukomo.
Ima kuhusu iwapo Marekani inaweza kufikia makubaliano ya madini na Ukraine wakati huu, Vance amesema ana imani makubaliano hayo yanaweza kufikiwa.
“Nafikiri Rais Trump bado ana azma ya kufikia makubaliano ya madini, na makubaliano hayo ni sehemu muhimu sana ya sera yake.”
Vance ameendelea kusisitiza kwamba wananchi wa Marekani wanastahili malipo kidogo ya uwekezaji mkubwa wa kifedha uliofanywa kwa Ukraine.
Kuhusu madai kwamba Marekani inaiwekea shinikizo kubwa Ukraine kuliko Russia na kwamba watu wanaweza kutarajia vikwazo zaidi vya Marekani dhidi ya Russia:
Makamu wa Rais Vance amesema halitakuwa jambo sahihi, akisema wanaamini msimamo wa Rais Trump ni kwa maslahi ya Russia, lakini pia kwa maslahi ya Ukraine na kwa maslahi mazuri ya Marekani kumaliza mgogoro huo.
#trump #zelenskyy #ukraine #russia #voa #makamurais #jdvance #msaada
6 Mar 2025
- The KUSCCO scandal has hit Saccos hard with 10 per cent of capital affected according to SASRA.
6 Mar 2025
- This is after the IEBC selection panel invited applicants for different positions including the chairperson and members.
6 Mar 2025
- In the new model, there will be a difference in how payments are made to health facilities.
6 Mar 2025
- This decision follows the tragic drowning of two students from Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT) just four days ago.
6 Mar 2025
- In a ruling on Thursday, the court also directed Ichung’wah to cover Omari’s legal costs.
6 Mar 2025
- The Ministry of Education has organised week-long meetings to discuss the implementation of the Competency-Based Curriculum (CBC) following its rollout in 2019.
6 Mar 2025
- Ex-journalist Moses Dola has been released after serving his 10-year sentence in prison for killing his wife Sarah Wambui Kabiru.
6 Mar 2025
- A police officer has been interdicted following Wednesday's shooting incident in Shauri Moyo area, whereby one person was killed.
6 Mar 2025
- Edward Mwai, the founder of Jesus Winner Ministry, has intimated that he has been receiving abusive phone calls from Kenyans after President William Ruto pledged a Ksh.120 million donation to his church.
6 Mar 2025
- Strongly backing Israel as a ceasefire teeters, Trump said he was "sending Israel everything it needs to finish the job" as his administration expedites billions of dollars in weapons.
6 Mar 2025
- The KUSCCO scandal has hit Saccos hard with 10 per cent of capital affected according to SASRA.
6 Mar 2025
- Raila is meeting party delegates from both counties at Kisii Agricultural Training Centre.
6 Mar 2025
- We apologize to Emmanuel Chebukati for any harm and embarrassment caused by the story.