Manusura waitaka serikali kulainisha malipo ya SHA

  • | KBC Video
    12 views

    Vuguvugu la mashirika ya kijamii linaitaka serikali kuweka mikakati ya dharura kuimarisha huduma za matibabu kwa wagonjwa wa saratani chini ya Halmashauri ya Afya ya Jamii, SHA. Hii inafuatia lalama za baadhi ya manusura wa saratani waliosimulia masaibu wanayopitia kutokana na ukosefu wa huduma na dawa ambazo zingeweza kuokoa maisha humu nchini. Kwenye kikao na wanahabari jijini Nairobi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Saratani Ulimwenguni, manusura hao walisema kwamba tangu mpito kutoka bima ya hazina ya kitaifa ya matibabu, NHIF hadi halmashauri ya SHA, fedha zilizotengwa kugharamia matibabu ya saratani humu nchini zimepungua kutoka shilingi laki sita hadi laki tatu kwa mwaka. Wanasema licha ya kulipia matibabu hitajika kwa kipindi cha miezi sita, hawajaweza kupokea dawa hizo katika hospitali za umma.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive