Goma DRC: M23 wasitisha vita... Matangazo ya Dira ya Dunia TV Jumanne 04/02/2025

  • | BBC Swahili
    6,906 views
    Kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda limetengaza kwamba limesitisha vita mashariki mwa DRC kwa misingi ya kibinadamu. Kundi hilo pia limesema kwamba halina nia ya kuteka au kudhibiti maeneo mengine ya mashariki mwa DRC. Tamko hili linaonekana kukinzana na lingine la awali kwamba wanalenga kuingia mji mkuu wa Kinshasa. Haya yanajiri wakati ambapo marais wa Rwanda na DRC wanatarajiwa kushiriki katika mkutano wa amani wa kikanda nchini Tanzania wikendi inayokuja ili kutafuta suluhu ya mzozo huo.