Mdau aishauri serikali namna ya kuongeza thamani mazao ya kilimo

  • | VOA Swahili
    7 views
    Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Amimza Cafe iliyoko Mkoa wa Kagera, Amiri Hamza, amesema kuwa bila maboresho ya sera, taifa litaendelea kushindwa kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. Amesema hayo katika mkutano wa tatu uliowakutanishi viongozi wa nchi 25 wanaozalisha zao hilo barani Afrika kuanzia tarehe 21-22, Februari, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es Salaam, Tanzania. Mkutano huu umeandaliwa na serikali ya Tanzania. Hamza amehimiza serikali na wadau kushirikiana kurekebisha sheria ili kuwapa vijana fursa zaidi kwenye sekta ya kahawa. “kufikia 2030 vijana wataweza kunufaika na zao la kahawa kwa ajira na mengineyo Kama tukibadilisha kanuni na sheria za mfumo wa fedha nchini, tusipo badili tutaendelea kuangaika na kulalamika kuhusu kuongeza thamani ya mazao yetu ya kilimo,” amesema Hamza Ili kuhakikisha sekta ya kahawa inachangia ipasavyo katika uchumi wa Afrika viongozi wa nchi 25 wameazimia kuhamasisha matumizi ya kahawa ndani ya bara na kuongeza ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi. Pia wamependekeza kuanzishwa kwa vituo vya umahiri na utafiti wa kahawa. Ripoti ya Amri Ramadhani, VOA, Tanzania. #tanzania #kahawa #amimzacafe #amirihamza #sera #serikali #voa #voaswahili #ushindani