Moto wa Palisade waleta uharibifu mkubwa maeneo ya Los Angeles

  • | VOA Swahili
    11 views
    Wakati upepo ukipungua kasi, wafanyakazi wa zima moto hatimaye wameanza kuudhibiti moto wa msituni ulioenea katika eneo la Pacific Palisades huko Los Angeles Ijumaa (Januari 10), kiwango kamili cha uharibifu kimeweza kuonekana kutoka angani. Mioto sita ya msituni iliyotokea kwa wakati mmoja imeteketeza maeneo jirani ya kauti ya Los Angeles tangu Alhamisi (Januari 7), imeuwa watu wasiopungua 10 na kuharibu takriban majengo 10,000. Baada ya kuwaka na kushindikana kudhibitiwa kwa siku kadhaa, licha ya juhudi za mamia ya wafanyakazi wa zima moto waliokuwa wakipambana na moto huo kutoka angani na ardhini, moto wa Palisades uliweza kudhibitiwa kwa asilimia 8. Cal Fire waliorodhesha viwango cha udhibiti kuwa ni asilimia 0 ilipofika Ijumaa. - Reuters #marekani #la #wildfires #voaswahili #santamonica #malibu